Monday, March 18, 2013

MAZUNGUMZO YA JINSI YA KUFANIKIWA MAISHANI

Katika Semina inayofanyika kila jumapili Nchi ya Ahadi (Sinza Kamanyola)
HARRIS KAPIGA 
Ndiye alikuwa mtoa mada na alizungumzia

"NIDHAMU YA MUDA"

Ambapo aliongelea kuhusu :Nini maana ya muda" akifafanua Muda ni kipindi ambacho vitu hutokea. Aligusia pia aina mbili za muda ambazo ni

1. Muda wa Saa, kwa mfano, dakika 60 ndani ya saa 1
2. Muda Halisi: hapa; hapa akimaanisha muda ulioko akilini, unaoweza kutengeneza wewe mwenyewe akilini na waweza umiliki. Vilevile aligusia swala la matumizi ya muda ambayo ni
  • Kufikiri: Inashauriwa kufikiri mawazo yaliyochanya na pia penda kuwa karibu na kitabu ambacho utakua unaandika mawazo yako
  • Mazungumzo: Hapa anashauri usipoteze muda wako mwingi ukiwa katika hali hii.
  • Vitendo: Harris anashauri penda kujiuliza "Toka umeamka umefanya nini" 
Pia akatoa dondoo kadhaa za kukuwezesha kutumia muda wako ambazo ni
1. Andika ratiba ya vitu utakavyofanya kwa siku
2. Pangilia muda maalum kwa kila shughuli ulizopangilia kufanya
3. Hakikisha 50% ya shughuli zitakazoleta manufaa kwako
4. Tenga dakika 30 kupanga ratiba ya siku
5. Usione aibu kusema "Usinisumbue nina kazi"
6. Pangilia muda wa kupokea simu, kujibu text na matumizi yako ya mitandao ya kijamii
7. Hakikisha shughuli utakachofanya katika mda wako kiwe kina manufaa kwako kwa asilimia 80
HARRIS KAPIGA

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...